Maswali yaulizwayo mara kwa mara

mwanachama.ccm.or.tz ni tovuti inayomsaidia mwanachama aliyesajiliwa kielektroniki kuangalia taarifa zake za uanachama alizosajiliwa nazo.

Taarifa zinazopatikana katika tovuti ya mwanachama.ccm.or.tz baada ya kuingia ni taarifa binafsi, taarifa za kiuanachama, malipo ya ada, michango, maelekezo jinsi ya kulipia ada za uwanachama, kurudisha risiti, kubadili neno la siri(nywila) na kutafuta namba yako ya uwanachama kama umesahau na pia unaweza kuwatafutia marafiki zako.

Bonyeza Ingia, ingiza namba ya uwanachama mfano C0000-0001-023-1, ingiza neno lako la siri ambalo ni jina lako la mwisho kama hujawahi kubadili, kisha bonyeza Ingia.

Kama hauna namba ya kieletroniki unaweza kujisajili na kupata namba yako ya kielektroni papo hapo kwa kubonyeza Jisajili kisha utapelekwa kwenye tovuti kuu ya chama ccm.or.tz na kuletewa ukurasa wa kujaza taarifa zako binafsi na za uwanachama. Ukimaliza Bonyeza Tuma kisha usajili wako ukikamilika utapata ujumbe mfupi wa maneno (SMS) ukikufahamisha namba yako mpya ya kieletroniki.

Kulingana na Katiba ya Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM), mwanachama hai ni yule anayelipa ada yake ya uwanachama ndani ya muda.

Unaweza kulipa ada yako ya uwanachama kielektroniki kwa kufuata maelekezo yaliyopo kwenye ukurasa wa Jinsi ya kulipia ada.
Kwa msaada zaidi

Kwa msaada zaidi unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255734398138 kwa kutuma ujumbe mfupi wa kawaida, WhatsApp au kupiga simu. Unaweza pia kutuandikia barua pepe.

ictsupport@ccm.or.tz
2024 © CCM.
TEHAMA HQ